MWAKA WA MT. YOSEFU


MWAKA WA MT. YOSEFU

Maadhimisho ya Mwaka wa Mtakatifu Yosefu yalizinduliwa tarehe 8 Desemba 2020 na yanatarajiwa kufungwa rasmi kwa kudema hapo tarehe 8 Desemba 2021. 

Baba Mtakatifu Francisko katika Waraka wake wa Kitume “Patris Corde” yaani “Kwa Moyo wa Kibaba”: “Mwaka wa Mtakatifu Yosefu, Kumbukumbu ya Miaka 150 Tangu Mtakatifu Yosefu alipotangazwa Kuwa Msimamizi wa Kanisa la kiulimwengu” anataja sifa kuu za Mtakatifu Yosefu akisema kwamba ni: “Baba mpendevu, mwenye huruma na mapendo; mtiifu na mwepesi kukubali. Ni Baba aliyebahatika kuwa na kipaji cha ugunduzi na ujasiri, lakini alibaki akiwa amefichwa kwenye vivuli, akawajibika na kuwa ni chanzo cha furaha na sadaka binafsi katika maisha.

Katika moyo wa unyenyekevu, Mtakatifu Yosefu aliyahifadhi mafumbo yote ya maisha yaliyomzunguka Mtoto Yesu na Mama yake Bikira Maria. Mtakatifu Yosefu mtu wa busara na haki, alijiaminisha mbele ya Mwenyezi Mungu na kuyatekeleza yale yote aliyoambiwa na Malaika katika ndoto.

 Lengo la maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu Yosefu anasema Baba Mtakatifu, ni kuwasaidia waamini kumfahamu na kumpenda Mtakatifu Yosefu aliyekuwa na mang’amuzi ya kibinadamu kama walivyo waamini wengi duniani. Ni Mtakatifu ambaye hakushtushwa sana na mambo, hakuwa na karama maalum wala kati ya watu wa nyakati zake, hakuwa mtu mashuhuri. Na wala Maandiko Matakatifu hayaoneshi maneno yaliyotoka kinywani mwake hata kidogo, lakini machoni pa Mwenyezi Mungu, aliweza kutenda matendo makuuu katika maisha na utume wake.

Mtakatifu Yohane Paulo II katika Waraka wake wa Kitume, “Redemptoris custos”, yaani “Mlinzi wa Mkombozi” uliochapishwa kunako tarehe 15 Agosti 1989 anamtaja Mtakatifu Yosefu kuwa ni Mlinzi wa Mkombozi na Familia Takatifu. Mtakatifu Yosefu alikuwa ni mtu mwenye imani thabiti, aliyejiaminisha mbele ya Mwenyezi Mungu. 

Mwanadamu anapomweka Mungu pembeni mwa mipango na vipaumbele vya maisha yake, matokeo ni kutumbukia katika majanga yanayodhalilisha utu, heshima na haki msingi za binadamu. Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko ameiridhia mabadiliko ya Nyongeza Katika Litania ya Mtakatifu Yosefu, yaliyowasilishwa kwake na Baraza la Kipapa la Ibada, Nidhamu na Sakramenti za Kanisa!

Tayari mabadiliko haya yamekwisha kutumwa kwa Marais wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki sehemu mbalimbali za dunia, ili yaweze kuingizwa katika Litania ya Mtakatifu Yosefu kwa kuzingatia maana. Mlinzi wa Mkombozi, Mhudumu wa Kristo, Mlinzi wa afya, Msaada wa wenye shida, Mlinzi wa wakimbizi, Mlinzi wa wenye shida na Mlinzi wa maskini.

Tunapoadhimisha Mwaka huu kwa maombezi ya Mt. YOSEFU,tuzikabidhi familia ,wito na wanyonge wetu katika jamii kwa Mungu.

Asante kwa kusoma katika tovoti wangu. Shemasi Nyonje anakutakia baraka na Amani.

Rev. Deacon. Nyonje ( Catholic Diocese of Nakuru- Kenya )0704603297.

Comments

Popular posts from this blog

NIMEKOSA Lyrics

SADAKA YANGU- Fr. Kauki

DIVINE MERCY