SADAKA YANGU- Fr. Kauki
SADAKA YANGU- Fr.Kauki
Chorus: Sadaka yangu, kwako ee Mungu
Ni moyo mnyofu na uliopondeka
(Tazama wapendezwa na kweli ya moyo
Nawe wanijulisha hekima kwa siri
Nioshe kabisa na uovu wangu wote
Na kinywa changu kitanena sifa zako) x2
1. Maana wewe Bwana hupendezwi
Na dha-bihu za kuteketezwa
Ama- sivyo mimi ningalikutolea
2. Wapendezwa na dhabihu za haki
Kuto-ka- kwa moyo mnyofu
Zitolewazo juu ya madhabahu yako
3. Ee Mungu wa wokovu wangu
Unipe moyo radhi wa utii
Usiniondolee Roho wako Mtakatifu
Comments