LITANIA YA MT. YOSEFU
LITANIA YA MT. YOSEFU
Bwana utuhurumie - Bwana utuhurumie
Kristo Utuhurumie - Kristo Utuhurumie
Bwana utuhurumie - Bwana utuhurumie
Kristo utusikie - Kristo utusikilize
Bwana wa Mbinguni, Mungu - utuhurumie
Mwana, Mkombozi wa dunia Mungu - utuhurumie
Roho Mtakatifu, Mungu mmoja - utuhurumie
Utatu Mtakatifu - utuhurumie
Maria Mtakatifu - utuombee
Yosefu Mtakatifu - utuombee
Mzao bora wa Daudi - utuombee
Mwanga bora wa Mababu - utuombee
Mume wa Mzazi wa Mungu - utuombee
Mlinzi wa Mkombozi - utuombee
Mlinzi safi wa Bikira - utuombee
Mlishi wa Mwana wa Mungu - utuombee
Mkingaji mwaminifu wa Kristo - utuombee
Mhudumu wa Kristo - utuombee
Mlinzi wa afya - utuombee
Mkubwa wa jamaa takatifu - utuombee
Yosefu mwenye haki - utuombee
Yosefu mwenye usafi wa Moyo - utuombee
Yosefu mwenye utaratibu - utuombee
Yosefu hodari kabisa - utuombee
Yosefu mtiifu kabisa - utuombee
Yosefu mwaminifu kabisa - utuombee
Kioo cha uvumilivu - utuombee
Mpenda umaskini - utuombee
Mfano wa watu wa kazi - utuombee
Uzuri wa mwendo wa nyumbani - utuombee
Mlinzi wa Mabikira - utuombee
Tegemeo la jamaa - utuombee
Msaada wa wenye shida - utuombee
Kitulizo cha maskini - utuombee
Matumaini ya wagonjwa - utuombee
Mlinzi wa wakimbizi - utuombee
Mlinzi wa wenye shida - utuombee
Mlinzi wa maskini - utuombee
Mlinzi wa walio kufani - utuombee
Mlinzi wa wenye kuzimia - utuombee
Kitisho cha mashetani - utuombee
Mlinzi wa Kanisa Takatifu - utuombee
Mwana Kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia utusamehe Bwana
Mwana Kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia utuhurumie Bwana
Mwana Kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia utusikilize Bwana
K. Amewekwa Bwana wa nyumba yake
W. Na mkubwa wa mali yake yote.
Tuombee: Mungu uliyetaka kwa maongozi yasiyotajika, ulimteua Yosefu mwenye heri, kuwa mchumba wa mzazi wako Mtakatifu, fanyiza twakuomba, tustahili kumpata mwombezi mbinguni yeye mwenyewe tunayemheshimu kama msimamizi duniani unayeishi na kutawala milele na milele. Amina.
( Sala hii Pamoja na nyongeza Mpya ya LITANIA ya Mtakatifu YOSEFU ilivyoongezwa na Papa Francisco imenakiliwa kutoka tovuti ya: https://www.vaticannews.va/sw/pope/news/2021-05/mwaka-mtakatifu-yosefu-nyongeza-litania-mtakatifu-yosefu-2021.html)
Mie wako. Shemasi Nyonje ( Jimbo Katoliki Nakuru- Kenya 0704603297)
Comments