Posts

Showing posts from June, 2021

SADAKA YANGU- Fr. Kauki

Image
SADAKA YANGU- Fr.Kauki Chorus: Sadaka yangu, kwako ee Mungu Ni moyo mnyofu na uliopondeka (Tazama wapendezwa na kweli ya moyo Nawe wanijulisha hekima kwa siri Nioshe kabisa na uovu wangu wote Na kinywa changu kitanena sifa zako) x2 1. Maana wewe Bwana hupendezwi     Na dha-bihu za kuteketezwa     Ama- sivyo mimi ningalikutolea 2. Wapendezwa na dhabihu za haki       Kuto-ka- kwa moyo mnyofu Zitolewazo juu ya madhabahu yako 3. Ee Mungu wa wokovu wangu Unipe moyo radhi wa utii Usiniondolee Roho wako Mtakatifu

NIMEKOSA Lyrics

Image
NIMEKOSA NIHURUMIE Chorus: Nimekosa, nimekosa, nimekosa Baba nimekosa nihurumie 1. Nimeyasema yasiyofaa ( kwako) Nimeyatenda yasiyofaa (Baba) Nimekosa ( nimekosa) nihurumie 2. Nimeyaona yasiyofaa (tena) nimesikia yasiyofaa (Baba) Nimekosa (Nimekosa) nihurumie 3. Kwa sababu ya matendo yangu (haya) jina lako latukanwa bure (Baba) Nimekosa (Nimekosa) nihurumie 4. Ninaleta familia yangu (kwako) ninayatubu makosa yao (yote) Nimekosa (Nimekosa) nihurumie 5. Ninaleta Kanisa lote (kwako) ninawaleta na viongozi (wake) Nimekosa (Nimekosa) nihurumie